Chelsea kwa Barca, Real na PSG hapatoshi

Muktasari:

Mechi za mtoano zitafanyika kuanzia Februari mwakani ikiwa ni hatua ya mtoano

Nyon, Uswisi. Chelsea imetupwa kwa Barcelona katika hatua 16 bora ya Ligi ya Mabingwa, wakati mabingwa watetezi Real Madrid wakipagwa kwa Paris-St-Germain.

Manchester City imepewa wapinzani dhaifu kidogo kulinganisha na wenzake katika Ligi Kuu England ikipangwa kucheza dhidi ya mabingwa wa Uswisi, Basel.

Manchester United inakupushia fainali ya msimu uliopita Europa Ligi kwa kupangwa dhidi ya Sevilla itaanza mechi yake ugenini.

Tottenham watakuwa na kibarua kizito ugenini wakati watakapowavaa  Juventus, wakati Liverpool wataonyeshana kazi na Porto katika ratiba hiyo iliyopagwa Nyon.

Japokuwa kwa sasa mashabiki Chelsea hawana wasiwasi sana, pamoja na kipigo cha mwishoni mwa wiki kutoka kwa West Ham, lakini wanajivunia rekodi nzuri dhidi ya Barcelona inawabeba.

Nyota wa miamba hiyo ya Catalan, Lionel Messi hajawahi kufunga dhidi ya Chelsea katika michezo nane aliyocheza dhidi ya yao ikiwa ni rekodi mbaya zaidi kwa mshambuliaji huyo.

 

Ratiba kamili

Juventus vs Tottenham

FC Basel vs Manchester City

FC Porto vs Liverpool

Sevilla vs Manchester United

Real Madrid vs Paris Saint-Germain

FC Shaktar Donetsk vs AS Roma

Chelsea vs Barcelona

Bayern Munich vs Besiktas