Kuna shida Stand United

Muktasari:

Stand ndiyo timu inayoburuza mkia baada ya kuvuna pointi saba katika mechi 12, jambo
linalowaumiza kichwa viongozi wa timu hiyo wafanye nini ili wasishuke daraja.

MATARAJIO ya klabu ya Stand United 'Chama la Wana' kufanya vizuri kwenye mzunguko wa pili baada ya kusajili wachezaji wapya kwenye dirisha dogo, bado ni ya kusuasua na sasa wana hali mbaya acha.
Stand ndiyo timu inayoburuza mkia baada ya kuvuna pointi saba katika mechi 12, jambo
linalowaumiza kichwa viongozi wa timu hiyo wafanye nini ili wasishuke daraja.
Katibu Mkuu wa Stand, Kenny Nyangi amesema walichotegemea baada ya dirisha dogo  la usajili, kungekuwa na mabadiliko ya haraka,  lakini wakafungwa mabao 3-0 Azam FC.
"Kiukweli tunapambana kadri tunavyoweza ili kuona timu haishuki daraja, tuna hali ngumu kupita watu wanavyojua, matokeo hayajawa mazuri kwetu," amesema Nyangi
"Kilichotuumiza ni usajili wa mwanzo wa msimu, tuliwaamini wale vijana mwisho wa siku tumevuna maumivu, ila tunaendelea kupambana."