Cannavaro: Yanga imeanza safari ubingwa

Muktasari:

Beki huyo ameichezea Yanga kwa zaidi ya miaka 10 sasa na kufanikiwa kutwaa mataji kadhaa ya Ligi Kuu Bara

Dar es Salaam. Beki mkongwe na nahodha wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro' amerudi ndani ya kikosi hicho na bahati, na amesisitiza safari ya mafanikio ndiyo wameianzisha ni ushindi mwanzo mwisho.

Cannavaro ambaye kwa kipindi kirefu alikuwa benchi kutokana na ushindani, lakini sasa amerudi kikosini hapo kama mwenye bahati kutokana na ushindi wa mabao 5-0 waliopata dhidi ya Mbeya City.

Cannavaro alisema: "Ni jambo zuri kupata matokeo mazuri, kwetu ni nzuri na nafasi  ya kutetea ubingwa wetu wa ligi. Tumeanza kwa kasi ambayo nafikiri itatuweka mahali salama."

Kuhusu kasi ya kufunga mabao mengi waliyoanza nayo Yanga sasa,  Cannavaro alisema, ndiyo wameanza safari na ni mwendo wa kupambana mpaka kieleweke.

"Ushindi wa mabao mengi ndiyo wenyewe, nafiki mashabiki na wapenzi ni muda wao wa kuiamini timu yao na kuiunga mkono ili tufanikiwe zaidi," alisema beki huyo.