Bocco aikamia Asante Kototo

Muktasari:

Bocco msimu uliopita alifunga mabao 14 katika Ligi Kuu Bara akiwa nafasi ya pili nyuma ya Emmanuel Okwi aliyefunga mabao 20

Dar es Salaam.Baada ya kukose mechi zote mbili za kirafiki walizocheza nchini Uturuki, Nahodha wa Simba, John Bocco ameweka wazi kuwa anatarajia kuwasha moto katika mchezo wao dhidi ya Asante Kototo katika Simba Day.

Bocco hakucheza katika mechi ya kwanza waliopata sare ya bao 1-1 dhidi ya Mouloudia na ule wa pili walishinda 3-1dhidi ya Umoja wa Madereva Teksi ya FC E Ksaifa.

Bocco, alisema alishindwa kucheza katika michezo hiyo kutokana na kuendelea kuuguza majeraha yake aliyoyapata katika mashindano ya Ligi msimu ulioisha na kuweka wazi kuwa sasa yupo fiti.

 "Ni kweli michezo yote nilikaa benchi sikucheza hata dakika tano mashabiki wangu wakae tayari kwaajili ya mchezo wetu Jumatano hii nitawasha moto wa ujuzi mpya kutoka kwa benchi letu la ufundi ambalo kwa asilimia kubwa lina makocha wewngi wapya," alisema Bocco.

"Huko tumepata mbinu za ziada hususani kwenye eneo la mazoezi ya viungo, kocha wetu mpya kwa kutumia vifaa vya kisasa kwenye kambi tuliyokuwa tumefikia ametufundisha mambo mengi na kila kitu kimebadilika nadhani mtaona katika mchezo wetu wa kwanza wa ushindani dhidi ya Asante Kotoko'', alisema Bocco.