VIDEO-Bocco nje, Mandawa ndani Taifa Stars

Muktasari:

  • Taifa Stars ina michezo miwili ya kirafiki dhidi ya Algeria na DR Congo

Kocha wa Taifa Stars, Salum Mayanga amemwita mshambuliaji Rashid Mandawa kuzipa pengo la John Bocco alijitoa kwa sababu ya kuumia.

Bocco aliumia wakati akichezea Simba katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Masry uliofanyika mwishoni mwa wiki.

Kocha Mayanga alisema amemuongeza Mandawa katika kikosi chake kuziba mapengo ya kukosekana kwa Bocco na Thomas Ulimwengu katika kikosi chake kitakachocheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Algeria na DR Congo.

Mandawa amekuwa katika kiwango cha juu katika kikosi cha BDF IX akiwa amefunga mabao 11, katika Ligi Kuu Botswana.

Wachezaji wengine waliongezwa katika kikosi hicho ni Himid Mao na Shabani Chilunda wa Azam kuchukua nafasi za Ulimwengu na Farid Mussa walioachwa Stars kutokana na sababu mbalimbali.

Mshambuliaji Ulimwengu wa SK Sloboda ameshindwa kujiunga na timu hiyo kutokana na kuangaikia kibali cha chake cha kazi, Bosnia.

Wakati Farid Mussa wa Tenerife hakupata ruhusa na Hamis Abdallah wa Sony Sugar ya Kenya kutokana na matatizo ya kiufundi.