Bocco, Okwi watajwa kuibeba Simba msimu huu

Wednesday May 16 2018

 

Msemaji wa Simba, Haji Manara amesema kwamba wachezaji Emmanuel Okwi na John Bocco wanastahili pongezi za kipekee kutokana na kuisaidia timu hiyo kufunga mabao mengi.

Mganda huyo hadi sasa amefikisha mabao 20, huku Bocco akiwa amefunga 14.

Okwi na Bocco ndio wachezaji ambao walikuwa wanachuana zaidi kwenye kasi ya ufungaji mabao katika mechi za ndani na nje ya Dar es Salaam.

Bocco na Okwi walikuwa na muunganiko mzuri ambao uliwawesha mmoja wao au wote wanapofunga kwa mechi za nyumbani wakati mwingine kufunga mechi za ugenini.

Ushindi mfululizo wa Simba umekuwa chachu kwa Wekundu hao wa Msimbazi kutawazwa mabingwa hata kabla ya kukamilisha mechi zao.