Bieber anaswa na kimwana mpya kabisa

Muktasari:

Bieber na kimwana huyo aliyefahamika kwa jina Baskini Champion walionekana kuwa pamoja kwenye shoo ya Craig David.

WIKI chache baada ya kupeana mapumziko na mpenzi wake Selena Gomez, mwanamuziki Justin Bieber ameonekana na kimwana mpya.

Bieber na kimwana huyo aliyefahamika kwa jina Baskini Champion walionekana kuwa pamoja kwenye shoo ya Craig David.

Bila wasiwasi, wawili hao walionekana wakicheza muziki huku muda wote mkono wa Bieber ukiwa kiunoni mwa kimwana huyo.

Hadi sasa haieleweki kama Bieber na Selena wameamua kuachana rasmi au ndiyo bado wapo kwenye mapumziko.

Taarifa ya waliyoitoa wawili hao ilidai wameamua kupumzisha uhusiano wao ili kumpa nafasi kila mmoja afanye mambo yake lakini bado hawajaachana.