Biashara United yamsainisha mkataba beki kisiki

Muktasari:

  • Kabla ya kujiunga na Biashara United, Mlinzi  huyo kisiki alikuwa akikipiga kwenye klabu ya Toto Africans ya jijini Mwanza na alikuwa mmoja wa wachezaji waliipandisha Ligi Kuu timu hiyo.

BIASHARA United imefanikiwa kumsainisha mkataba wa Miaka miwili beki wake wa kati, Lameck Machumu ambaye aliweza kuipandisha Ligi Kuu timu hiyo msimu ujao.
Kabla ya kujiunga na Biashara United, Mlinzi  huyo kisiki alikuwa akikipiga kwenye klabu ya Toto Africans ya jijini Mwanza na alikuwa mmoja wa wachezaji waliipandisha Ligi Kuu timu hiyo.
Meneja wa klabu hiyo, Aman Josia alisema wameamua kumpa mkataba mpya beki huyo ili aweze kuimarisha safu ya ulinzi ya kikosi kwenye kwenye msimu ujao wa Ligi Kuu.
“Machumu amesaini mkataba wa miaka miwili na bado tupo kazini kwani tunataka kutengeneza kikosi bora ambacho kitaleta ushindani kwenye Ligi Kuu msimu ujao,” alisema Josia.
Kwa upande wake beki Machumu alisema atapambana kwa kushirikiana na wachezaji wenzake ili timu hiyi iweze kufanya vyema kwenye Ligi Kuu msimu ujao kama tulivyofanya vizuri kwenye Daraja la Kwanza.
Alisema baada ya kupewa mkataba huo kwa sasa atajituma kuhakikisha anapata namba kwenye kikosi cha kwanza kwani bila ya kufanya hivyo anaweza kuishia benchi.
“Niwashukuru viongozi kwa kunipa mkata mwingine niwakikishie nitajituma kuanzia kwenye mechi hadi mazoezini ili kuipa mafanikio Biashara United,” alisema Machumu.