Beki wa Azante Kotoko aitamani Azam

Muktasari:

  • Nafiu aliichezea Azam ambayo ni mabingwa wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2013-2014.

Dar es Salaam. Beki wa zamani wa Azam FC, Nafiu Awudu amekuja nchini na Asante Kotoko  ya Ghana lakini bado anatamani kurudi ndani ya kikosi hicho.

Nafiu aliichezea Azam ambayo ni mabingwa wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2013-2014.

Baada ya mchezo huo, Nafiu alitamani zaidi kupata taarifa za klabu hiyo kocha na baadhi ya wachezaji anaowajua.

Amesema: "Nipo na Asante Kotoko lakini Azam naikumbuka. Suala la kurudi tena si mbaya bado natamani."

Nafiu alisajiliwa na kucheza Juni 2011 pamoja na mshambuliaji mwingine kutoka Ghana Wahabu Yahya hata hivyo wachezaji  hawakudumu kutokana na ushindani wa namba uliokuwepo kikosini hapo.

Asante Kotoko ilikuja na kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Simba katika maadhimisho ya siku yao ya Simba Day.