Beki wa Simba atimkia Rayon Sports

Saturday January 13 2018

 

By MWANAHIBA RICHARD

AliyekuwaA beki wa Simba, Janvier Bokungu yupo mbioni kujiunga na Rayon Sports baada ya kufanya majaribio na miamba hiyo ya Rwanda.
Bokungu aliichezea Simba msimu uliopita kabla ya kumtupia virago madai ya kwamba umri wake mkubwa pamoja na kiwango chake kutokuwa cha kuridhisha.
Bokungu alitua katika kikosi hicho wiki hii na kuanza majaribio yake ambapo Msemaji wa klabu hiyo,  Gakwaya Olivier alisema kuwa maamuzi yote ya kumsajili wamemuachia kocha wao.