Beki Mstaarabu aibukia Copa Umisseta

Muktasari:

  • Beki huyo hadi wachezaji wenzake wanamuonea wivu kutokana na kiwango chake na nidhamu aliyonayo hadi waamuzi wanaochezesha mashindano hayo wamempachika jina la Beki Mstaarabu.

Mwanza. Katika ya vitu wanachojivunia timu ya soka ya jiji la Dar es Salaam katika mashindano ya Copa Umisseta ni kiwango bora cha beki wake, Kija Kassian.
Beki huyo hadi wachezaji wenzake wanamuonea wivu kutokana na kiwango chake na nidhamu aliyonayo hadi waamuzi wanaochezesha mashindano hayo wamempachika jina la Beki Mstaarabu.
"Huyu beki dakika zote 90 hachomoi jezi, anajua mpira, hata katika uchezaji wake hana faulo za kijinga, pasi zake zimepimwa na hana mambo mengi uwanjani," alisema mmoja wa waamuzi wa mashindano hayo.
Kija mwenyewe anakwambia amelisikia jina hilo lakini hakujua chanzo cha kuitwa beki mstarabu ni nini?.
Dar es Salaam ndiyo bingwa mtetezi wa mashindano hayo upande wa Soka la wasichana na Jana jioni waliongeza pointi kwa kuifunga Geita mabao 4-0 huku 'Beki Mstaarabu' akifunga moja na Joyce Meshack akifunga matatu.