Beki Mnyarwanda Singida United aanza kulisoma soka la Bongo

Muktasari:

Beki huyo tegemeo wa timu ya Taifa ya Rwanda 'Amavubi', alijiunga klabuni hapo akitokea APR ya Rwanda ambapo tangu ameanza kukichezea kikosi hicho.

BEKI Mnyarwanda wa Singida United, Michel  Rusheshangoga amesema, mechi tatu walizocheza zimemfanya auelewe mpira wa Tanzania na sasa hana presha.

Beki huyo tegemeo wa timu ya Taifa ya Rwanda 'Amavubi', alijiunga klabuni hapo akitokea APR ya Rwanda ambapo tangu ameanza kukichezea kikosi hicho.

"Singida tuna timu nzuri, kilichokuwa kinatusumbua awali ni ugeni, lakini sasa mambo ni mazuri, hakuna kinachosumbua tena tunajua ni mpira wa aina gani tunaotakiwa kucheza ili tupate matokeo mzuri," alisema Michel.