Beki Kabanda aongezewa miaka miwili Mbeya City

Muktasari:

Kabanda amesema kuongeza kwake mkataba kwenye timu hiyo ya kizazi kipya kutampa nafasi ya  kuendelea kushirikiana na wachezaji wenzake ili kuipa mafanikio zaidi.

Dar es Salaam. Klabu  ya Mbeya City imemuongezea mkataba wa miaka miwili beki, John Kabanda  ambaye yupo kwenye kikosi hicho tangu 2013.

Kabanda amesema kuongeza kwake mkataba kwenye timu hiyo ya kizazi kipya kutampa nafasi ya  kuendelea kushirikiana na wachezaji wenzake ili kuipa mafanikio zaidi.

“Mbeya City sio timu ndogo, ni moja ya timu shindani kwenye ligi, nitajitahidi kutoa mchango wangu kwa kushirikiana na wachezaji wenzangu ili kufanya vizuri.” alisema Kabanda.

Kaimu ofisa habari wa timu hiyo, Shah Mjanja aliongeza  kuwa kikosi hicho bado kinaendelea kuimarishwa ili kiwe na kasi  kubwa ya ushindani tofauti na msimu uliopita.