Beki Azam afurahia maisha Tanzania

Dar es Salaam. Beki wa Azam, Daniel Amoah amefunguka akisema anafurahia maisha ya Bongo na anatamani kuendelea kucheza soka la kulipwa hapa nchini.

Amoah mwenye uwezo wa kudumu kucheza katika kikosi cha kwanza cha Azam, alisema maisha ya Tanzania ni mazuri kama kwao Ghana na haoni shida kuendelea kucheza hapa.

Beki huyo aliyejiunga na Azam mwishoni mwa mwaka jana kwa mkataba wa miaka mitatu, alisema kwa sasa anajifunza lugha ya kiswahili ili aweze kuwasiliana vizuri na wananchi wanaoizunguka jamii yao.

"Nafurahi kuwa hapa, maisha ni mazuri sana. Nimeanza kujifunza kiswahili kidogo kidogo," alisema Amoah.