Namba yamtesa beki Singida

Muktasari:

Chuku pamoja na kiungo,  Yusuph Kagoma ni wachezaji pekee kutoka kwenye kikosi cha Singida United ambao wameitwa Kilimanajro Warrios ambacho kitashiriki mashindano ya Olimpic  yanayotarajiwa kuanza  Julai 22 hadi  Agosti 8, 2020  nchini  Japan.

Beki wa kushoto wa  timu ya Taifa chini ya umri wa miaka 23 ‘Kilimanjaro Warrios’, Salum Chuku (20) amekiri kukabiliwa na changamoto ya kupata nafasi kikosi cha  kwanza katika klabu yake ya Singida United.
Chuku pamoja na kiungo,  Yusuph Kagoma ni wachezaji pekee kutoka kwenye kikosi cha Singida United ambao wameitwa Kilimanajro Warrios ambacho kitashiriki mashindano ya Olimpic  yanayotarajiwa kuanza  Julai 22 hadi  Agosti 8, 2020  nchini  Japan.
“Chaguo namba moja la mwalimu  kwenye kikosi cha kwanza  ni Shafik Batambuze, kwangu ni changamoto ambayo imekuwa ikiniumiza kichwa kama mchezaji mwenye shauku ya kutaka nafasi ya kucheza  kikosi cha kwanza, nachofanya nikuendelea kujituma,"alisema Chuku.
“Nomba Mungu nisipate majeraha, kama nisipokuwa na majeraha inamaana nitaendelea kuwa kwenye mazingira mazuri ya kupigania nafasi na inawezekanakabisa kuwa mchezaji wa kudumu kikosi cha kwanza.”
Batambuze ambaye ni raia wa Uganda, ana umri wa miaka 23 na alijunga na Singida United mwanzoni mwa msimu huu wa 2017/2018  akitokea Tusker ya Kenya.