Barcelona yamnasa Paulinho kama utani

Muktasari:

  • Kiungo mwenye miaka 29, anakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Barcelona tangu miamba hiyo ya Hispania ilipouza  Neymar kwa Paris St Germain kwa uhamisho uliovunja rekodi ya dunia wa euro 222 milioni, jambo lililowafanya miamba hiyo ya Catalans kusaka wachezaji wa kumalisha kikosi chake.

Barcelona amefikia makubaliano na klabu ya Guangzhou Evergrande ya kumnunua kiungo Mbrazili Paulinho kwa euro 40 milioni ilisema taarifa ya klabu hiyo ya Hispania.

"Mchezaji huyo mpya wa Barcelona atasaini mkataba wa miaka mine na mchezaji mwenyewe amenunua mkataba wake kwa gharama ya euro 120 milioni," ilisema taarifa ya Barcelona.

"Paulinho atafanyiwa vipimo vya afya Alhamisi na atasaini mkataba pamoja na kutambulisha rasmi."

Kiungo mwenye miaka 29, anakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Barcelona tangu miamba hiyo ya Hispania ilipouza  Neymar kwa Paris St Germain kwa uhamisho uliovunja rekodi ya dunia wa euro 222 milioni, jambo lililowafanya miamba hiyo ya Catalans kusaka wachezaji wa kumalisha kikosi chake.

Kiungo wa Liverpool, Philippe Coutinho na chipukizi wa Borussia Dortmund, Ousmane Dembele wote wanataja kutakiwa na Barcelona ili kuzipa pengo la Neymar katika safu ya ushambuliaji.

Coutinho ameomba kuondoka Anfield.

Barcelona tayari mara mbili maombi yao ya kumtaka Coutinho yamekataliwa na sasa wanajiandaa kurudi kwa mara ya tatu kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari vya Hispania.