Barcelona yagawa kipigo Kombe la Copa del Rey

Friday January 12 2018

 

Hispania. Klabu ya Barcelona imeiangushia kipigo cha mabao 5-0 timu ya Celta Vigo, huku mshambuliaji Lionel Messi akiweka wavuni mabao yake mawili mchezo uliopigwa jana Alhamisi usiku.

Ushindi huo umeivusha Barcelona hatua ya robo fainali huku matokeo ya jumla ya kiwa 6-1 kutokana na mchezo wao wa awali kutoka sare ya bao 1-1.

Mabao ya haraka haraka ya Messi yaliwekwa wavuni dakika ya 13 na 15 kipindi cha kwanza yote akitengenezewa pasi na Jordi Alba.

Mabao mengine ya Barcelona yaliwekwa wavuni na Luis Suarez, Jordi Alba na Ivan Rakitic.