Barcelona yabadili gia, sasa kumsajili nyota wa Real Madrid

Friday August 11 2017

 

Hispania. Kocha wa Barcelona, Ernesto Valverde amerudi kwa nyota wa Real Madrid, Marco Asensio baada ya kumtengea dau la Pauni 72 milioni ili kuziba pengo la mshambuliaji wao waliyemuuza PSG, Neymar Jr.

Miamba hiyo ya Hispania, awali walitupa karata yao kwa mchezaji wa Liverpool, Philippe Coutinho ambaye uongozi wa klabu umegoma kumuuza.

Barcelona imeamua kurudi kwa Asensio (21) kutokana na kuwa na uwezo wa kutoa dau ambalo Real Madrid wameliweka kwa ajili ya kumuuza mchezo huyo.