Barca yamfanyia 'ntima nyongo' Neymar

Thursday August 10 2017

 

Barcelona, Hispania. Barcelona imekataa kuthibisha uhamisho wa Neymar kwenda PSG hadi watakapolipwa euro 222milioni.

Kutokana na sakata hilo Neymar sasa atalazimika kusubili zaidi kabla ya kuichezea Paris Saint-Germain katika mashindano mbalimbali.

Miamba hiyo ya Catalans wanatakiwa kutoa kibari cha uhamisho wa kimataifa ITC, lakini wamegoma kutoa hadi pale watakapopokea malipo yake yote kama walivyokubaliana.

Tayari ameshakosa mechi ya kwanza ya Ligue 1 kati ya PSG dhidi ya Amiens, pia kuna uwezekano Mbrazili huyo akaikosa mechi Jumapili dhidi ya Guingamp kama euro 222 milioni zitakuwa hazijalipwa katika akaunti ya Barcelona hadi wakati huo.