Barca yajipanga kuibomoa Bayern

Muktasari:

  • Barcelona ipo katika harakati za muda mrefu za kumsaka kiungo wa kumrithi Andrea Iniesta

Barcelona imeanza kumnyemelea kiungo wao wa zamani, Thiago Alcantara (26), anayekipiga Bayern Munich kama wakishindwa katika mbio zao za kumchukua kiungo wa Liverpool, Philippe Coutinho (25), katika dirisha la Januari.

Staa huyo wa kimataifa wa Hispania ambaye baba yake ni nyota wa zamani wa Brazil, Mazinho anataka kurudi Barcelona baada ya kuuzwa na klabu hiyo mwaka 2013 kwenda Ujerumani akimfuata kocha wake wa zamani wa Barcelona, Pep Guardiola.

Barcelona bado wanasaka mrithi wa muda mrefu wa mkongwe wao, Andres Iniesta ambaye siku zake za kucheza kiwango cha juu zimeanza kuhesabika huku wakimkosa Coutinho katika dirisha kubwa lililofungwa hivi karibuni.

Katika hatua nyingine Barcelona inawafuatilia mastaa watatu wa Bayer Leverkusen akiwemo beki wa kati, Jonathan Tah mwenye miaka 21.

Wengine ni pamoja na mawinga, Julian Brandt (21) na Leo Bailey (20), ambaye alitua katika timu hiyo dirisha la Januari mwaka huu akitokea Genk ya Ubelgiji na ana mkataba na timu hiyo mpaka mwaka 2022.