Bao la Yanga lampa kiroba cha mchele

Muktasari:

Sasa walichokifanya ni kumwagia zawadi za kila aina straika huyo aliyewalaza Yanga njaa wakati huu wakiifukuzia Simba kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara.

Dar es Salaam. Mashabiki wa Mbeya bana wana mzuka kinoma na bao la dakika za lala salama la mshambuliaji wa Mbeya City, Iddy Seleman 'Ronaldo' limewapagawisha kwelikweli.

Sasa walichokifanya ni kumwagia zawadi za kila aina straika huyo aliyewalaza Yanga njaa wakati huu wakiifukuzia Simba kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara.

Ronaldo amesema mashabiki wamemfanyia saprize ya maana kwa kumpa zawadi ya mchele, viazi, vitunguu, ndizi na pesa taslimu kama shukrani ya kupeleka msiba Jangwani.

"Nilikuwa nasikia kwa wachezaji wenzangu namna mashabiki wa Mbeya walivyowakarimu kama ukiwafurahisha, nilichokiona baada ya kurudi kambini, kilinishangaza kwelikweli. Mashabiki wameleta mchele, ndizi yaani ni mzuka mwingi," alisema.

Hata hivyo, Ronaldo hakutaka kuweka wazi kiasi cha pesa alichovuna kutoka kwa mashabiki hao.