Banka wa Simba yeye na biashara tu soka tupa kule!

Muktasari:

  • Banka ambaye anasafirisha biashara tofauti zaidi ikiwa ni nguo kutoka China, ameamua kujikita huko baada ya kupumzika kucheza soka.

Dar es Salaam. Kiungo wa zamani wa Simba na Yanga, Mohamed Banka amesema, hana mpango wa kucheza soka la ushindani na amegeukia  biashara ambayo inampa mafanikio kwa sasa.

Banka ambaye anasafirisha biashara tofauti zaidi ikiwa ni nguo kutoka China, ameamua kujikita huko baada ya kupumzika kucheza soka.

Awali alitarajia kurudi uwanjani lakini sasa hivi hana mpango huo kabisa na anafanya mazoezi yake binafsi kwa ajili ya kujenga mwili na burudani.

"Kwa sasa sina mpango kabisa wa kurudi uwanjani eti kwa ajili ya kucheza ligi ya ushindani, hapana kwa sasa akili zangu nimezielekeza kwenye biashara zangu tofauti,"alisema Banka.