Bonanza la kina Banka ni Mei Mosi

Muktasari:

(FFCC)  GYM, wameanda bonanza 'babu kubwa' litakalofanyika siku ya Mei Mosi mwaka huu katika Viwanja vya GYM hiyo maeneo ya Tabata Segerea.

KIUNGO wa zamani wa Simba, Mohamed Banka pamoja na wanachama wenzake wa Fitness Family Connection Club

(FFCC)  GYM, wameanda bonanza 'babu kubwa' litakalofanyika siku ya Mei Mosi mwaka huu katika Viwanja vya GYM hiyo maeneo ya Tabata Segerea.

Bonanza hilo ambalo litaanza saa 12 asubuhi na kumalizika saa sita mchana litafanyika katika viwanja hivyo ambapo pia, ndipo ilipo sheri ya mafuta ya Oil Com.

Katibu Mkuu wa Wanachama hao, Munir Said amesema, bonanza hilo ni kwa ajili ya kuweka miili sawa na yeyote anayetaka kushiriki anakaribishwa na kutakuwa na mazoezi tofauti ya Joging, Aerobic na Zumba.

"Maisha ya sasa bila mazoezi hayaendi magonjwa ni mengi na vifo vya ghafla vinavyosababishwa na kutofanya mazoezi vinatokea kila siku, hivyo sehemu ya bonanza hilo ni kuhamasisha watu tofauti wapende mazoezi na tunawakaribisha waje kuungana nasi bure bila gharama yoyote,"anasema Munir.

Anawataja baadhi ya walimu watakaoongoza mazoezi hayo ni pamoja na Emmanuel, Kashai, Andrew, Wile, Sadi, Deo, Najim, Ndanje, Chiko na mtaalamu wa Zumba anayeitwa Devi.

Hata hivyo, mbali na Banka wachezaji wengine wanaofanya mazoezi hapo ni pamoja na Juma Seif 'Makapu' , Haji Mwinyi wa Yanga,  Jerry Tegete wa Majimaji na Nizar Kharfan wa Sing