Balozi ampokea Samata Algeria

Muktasari:

Tanzania itacheza mechi ya kirafiki na Algeria ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mechi za kusaka kufuzu kwa AFCON 2019


Dar es Salaam. Nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta leo jioni amepokewa Balozi wa Tanzania nchini Algeria, Omar Yusuf kwenye Uwanja wa ndege wa Algiers kwa ajili ya kujiunga na wenzake.

Samatta ametua nchini humo akitokea Ubelgiji katika  klabu yake ya KRC Genk iliyoshindwa Jumamosi kutwaa ubingwa wa kombe la nchi hiyo kwa kufungwa na Standard kwa bao 1-0.

Taifa Stars imesafiri leo kuelekea nchini humo kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Algeria, Machi 22.

Nyota wengine wa Taifa Stars ambao wanategemewa kujiunga na timu hiyo nchini Algeria ni Shomari Kapombe, Shiza Kichuya, Aishi Manula, Erasto Nyoni wa Simba ambao walikuwa nchini Misri kwa mchezo wa marudiano dhidi ya Al Masry.

Pia, nahodha wa kikosi hicho, Mbwana Samatta ambaye anatokea Ubelgiji kwenye klabu yake ya KRC Genk pamoja na Rashid Mandawa wa BDF IX ya Botswana.

Mara baada ya mchezo huo, Stars itarejea nchini, Machi 24 kwa ajili ya kujiandaa na kucheza mchezo mwingine wa kirafiki Machi 27 dhidi ya DR Congo.