Bale hatihati kuondolea tuzo Ulaya

Muktasari:

  • Mshambuliaji huyo amekuwa akisumbuliwa na majeruhi ya mara kwa mara katika kikosi cha Real

Mshambuliaji Gareth Bale amejiweka katika mazingira magumu ya jina lake kubaki katika rekodi ya wachezaji bora UIaya.

Pia, ameweka rehani kibarua chake Real Madrid baada ya kutumia muda mrefu akiwa nje ya uwanja kutokana na majeraha.

Majeraha ya hivi karibuni ambayo yatakuweka nje ya dimba wiki sita, yamemuweka njia panda nyota huyo wa timu ya taifa ya Wales.

Maumivu ya misuli yamemkosesha nafasi ya kujiunga na Man United baada ya kocha  Jose Mourinho kudai hawezi kumsajili katika dirisha dogo la usajili Januari, mwakani.

Bale, mchezaji ghali wa zamani hana thamani tena na Real Madrid inaweza kumuuza kwa bei ya kutupa kwa klabu itakayomtaka.

Kiungo wa pembeni mwenye miaka 28, amekosa mechi 40 kati ya 60 zilizopita hatua inayomuweka katika mazingira magumu.

Endapo mshambuliaji huyo wa zamani wa Tottenahm Hotspurs atakuwa fiti, winga huyo anatajwa kuwa ni mchezaji mahiri mwenye uwezo mkubwa wa kucheza soka.