#WC2018: BINGWA KOMBE LA DUNIA: Ufaransa yaweka rekodi nzito ubingwa Russia

Muktasari:

Mwisho wa siku, michuano ya Kombe la Dunia 2018, imemalizika kwa kuishuhudia Ufaransa ikiingia katika vitabu vya historia kama taifa lililobeba taji hili mara mbili, wakiungana na Brazil, Ujerumani na Italia.

Kikosi cha Ufaransa kimeibuka bingwa wa fainali za Kombe la Dunia zilizohitiomishwa leo Jumapili kwenye dimba la Linhzniki jijini Moscow nchini Russia..
Mwisho wa siku, michuano ya Kombe la Dunia 2018, imemalizika kwa kuishuhudia Ufaransa ikiingia katika vitabu vya historia kama taifa lililobeba taji hili mara mbili, wakiungana na Brazil, Ujerumani na Italia.
Aidha ubingwa wa leo pia umeshuhudia Mbappe akivunja rekodi nyingine mbili za mkali wa soka, Mbrazil Pele. Mbappe alifunga moja ya mabao ya leo na kuvunja rekodi ya kuwa kinda aliyefunga kwenye mechi ya fainali ya Kombe la Dunia, akivunja rekodi ya Pele aliyoiweka mwaka 1958.
Rekodi nyingine iliyovunjwa na Mbappe leo ni kutwaa Kombe la Dunia akiwa na umri wa miaka 19 sawa na Pele (1958). Kocha wa Ufaransa Didier Deschamps, naye anaingia katika vitabu vya kumbukumbu, kwa kuweka rekodi ya kuwa mfaransa wa kwanza na kocha wa tatu kutwaa taji hili akiwa mchezaji (1998) na baadae akiwa Kocha (2018).
Wengine waliofanya hivyo ni Franz Beckenbeur na Mario Zagallo. Kama hiyo haitoshi, Ufaransa mbali na kuendeleza ubabe dhidi ya Croatia, Les Blues pia imeweka rekodi ya kutwaa taji hili, ikiwa na kikosi kichanga zaidi kwani ni mchezaji mmoja tu katika kikosi hicho cha mabingwa ndiye ana umri zaidi ya miaka 30, (Hugo Lloris).