B Band yanogesha tuzo Ligi Kuu

Mwanamuziki Banana Zorro na bendi yake ya B Band wameupamba usiku wa tuzo za Ligi Kuu Bara 2017/2018 zinazotolewa kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini.
Bendi hiyo ilianza kutumbuiza mnamo saa 2.50 wakati ambao wageni waalikwa walianza kupata chakula cha jioni.
Wanamuziki wa Bendi hiyo walianza na wimbo wa Malaika na kisha kuendelea na nyimbo nyingine.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe anatarajiwa kuongoza hafla ya utoaji Tuzo za Ligi Kuu Tanzania Bara 2017/2018 zinazofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City.