Azam itasajili wapya mpaka Kagame ipite

Muktasari:

Azam iliyo chini ya benchi jipya la ufundi linaloongozwa na  Mholanzi Hans Pluijm na Juma Mwambusi, limeshakamilisha usajili wa Wazimbabwe Donaldo

Dar es Salaam. Matajiri wa Azam FC wamesema, wataanza harakati za kufanya usajili wa wachezaji wengine mpaka mashindano ya Kombe la Kagame yamalizike.

Azam iliyo chini ya benchi jipya la ufundi linaloongozwa na  Mholanzi Hans Pluijm na Juma Mwambusi, limeshakamilisha usajili wa Wazimbabwe Donaldo

Ngoma na Tafadzwa Kutinyu, pia Nicholas Wadada raia wa Uganda na wazawa Ditram Nchimbi na Mudathir Yahya.

Wamesema, hao wachezaji walionao sasa ndiyo sehemu ya kikosi chao kamili,  kwa sasa wanasimamisha zoezi hilo mpaka mashindano hayo ya Kagame yatakapomalizika.

"Kusajili mpaka Kagame iishe, hapo ndipo tutaangalia mapungufu na kuyafanyia kazi, tunafanya hivi vitu kwa akili sana,"alisema mtu wa karibu wa Azam.

Azam ndiyo bingwa mtetezi wa Kombe la Kagame ambalo mechi zake zinachezwa Uwanja wa Taifa.