Azam yashika kombe mkono mmoja

Muktasari:

  • Mshambuliaji Shabaan Idd Chilunda alifunga bao la kuongoza dakika 32, akiunganisha kwa kichwa kona iliyopigwa na Bruce Kangwa.

Dar es Salaam. Mabingwa watetezi wa Azam FC wanakwenda mapumziko wakiwa mbele kwa bao 1-0 dhidi ya Simba katika mchezo ulioshudiwa na mashabiki wengi waliojitokeza kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Mshambuliaji Shabaan Idd Chilunda alifunga bao la kuongoza dakika 32, akiunganisha kwa kichwa kona iliyopigwa na Bruce Kangwa.
Katika mchezo huo mashabiki wa Simba ndio wengi kuliko wa Azam ambao baadhi wamevalia jezi za Yanga na wengine mavazi ya kawaida.
Vigoma na miruzi na kelele za hapa na pale kutoka jukwaa la mashabiki wa Simba na Azam FC vinasikika.
Mpaka dakika 25 timu zote mbili zinaonekana kushambuliana kwa zamu, huku ukichezwa kwa kasi ya juu na ubabe wa hapa na pale.