Azam ya Pluijm huko Uganda acha kabisa

Muktasari:

Pluijm ambaye Januari 3, mwakani atafikisha miaka 70, amesema katika mchezo huo uliokuwa na ushindani umemfanya atambue mapungufu ya timu na zaidi ilikuwa kwenye safu ya ulinzi.

Dar es Salaam. Kikosi cha Azam FC, kilishindwa kutamba mbele ya KCCA juzi Ijumaa na wakafungwa mabao 4-2, lakini kocha mkuu wa kikosi hicho Hans Pluijm amesema, timu inayoandaliwa huko Uganda ni tishio na anaendelea kufanyia kazi muungano wa timu, mbinu na umakini.

Pluijm ambaye Januari 3, mwakani atafikisha miaka 70, amesema katika mchezo huo uliokuwa na ushindani umemfanya atambue mapungufu ya timu na zaidi ilikuwa kwenye safu ya ulinzi.

"Tumefungwa, kwangu nahesabu mabao 2-0, lakini ulikuwa mchezo mzuri ambao umenifanya nitambue ni maeneo gani natakiwa kuyafanyia kazi zaidi,"anasema Pluijm kocha wa zamani wa Yanga na Singida United.

"Tatizo kubwa lilikuwa upande wa kuzuia, hakukuwa na muunganiko mzuri wa timu, umakini na mbinu na ndiyo maeneo ambayo naendelea kufanyia kazi kwa umakini."

Mholanzi huyo amesisitiza, vijana wanafanya kazi nzuri na wanapambana na amefurahia hali ya hewa ya nchi hiyo kuwa nzuri si joto wala baridi.

Ameeleza namna ambavyo faida wanayoipata katika kucheza mechi hizo na timu kubwa za Uganda.

"Nfurahia ushindani huo kulingana na aina ya timu tunazocheza nazo, tunachokipata itakuwa faida kwetu tutakaporudi nchini na kuanza kucheza mechi za ligi na mashindano mengine,"alisema Pluijm tunachokipata huku 

Azam imeweka kambi nchini Uganda kwa wiki tatu kujiandaa na msimu mpya wa ligi unaotarajia kuanza Agosti 22.