Azam wanahitaji ushindi wa jasho

Dar es Salaam. Kocha msaidizi wa Azam FC, Idd Cheche amesema wanahitaji mechi za ushindani zaidi ili wachezaji wao wapate ushindi wa jasho, utakaowafanya wawe na viwango vya kimataifa.

Cheche ameeleza kwamba malengo yao ni ubingwa, hivyo hawahitaji mtelemko utakaowafanya washindwe kuonyesha ushindani kwenye mashindano ya kimataifa mwakani.

"Kama wachezaji wanahudumiwa kwa kila kitu lazima watambue wazi wanahitaji kufanya kazi iliyowapelekea kuwepo kwenye klabu lasivyo watakuwa nje ya malengo waliyotarajiwa kutoka kwao

Baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Lipuli ya Iringa, Azam itakutana na Singida United, Jumamosi ya wiki hii kwenye Uwanja wa Jamhuri Dodoma.

Kocha huyo ameizungumia mechi hiyo haitakuwa rahisi kutokana na wapinzani wao watahitaji kuendeleza rekodi ya ushindi baada ya kuwafunga Kagera Sugar kwa bao 1-0.

"Kwanza timu ipo kwa kocha mwenye ujuzi mkubwa Hans Pluijm aliyeipa Yanga mataji mengi hivyo tutalazimika kutoa jasho kupata ushindi wa mechi hiyo," alisema Cheche.