Azam FC tukishindwa Yanga basi Simba

Wednesday June 13 2018

 

By Olipa Assa

Dar es Salaam.Vigogo wa Azam FC, hawalazi damu kuhakikisha wanafanikisha saini ya beki wa Yanga, Juma Abdul na endapo watashindwa basi watatua Simba.

Mmoja wa vigogo hao ambaye hakutaja kuweka wazi jina lake, anasema wana mhitaji wa beki namba mbili na ndicho kinachowafanya wapambane ili kumnasa staa huyo.

"Tukimshindwa Juma Abdul tutahamia upande wa pili yaani Simba kumchomoa anayecheza nafasi hiyo iwe kwa hali na mali au la tutaangalia mwenye ubora kwa timu zilizoshiriki Ligi Kuu kwa msimu huu," alidai mtoa habari huyo.