Aslay awaomba msamaha Wazanzibar

Muktasari:

  • Mkuu wa mkoa huyo, ametoa katazo kwa Aslay kufanya shughuli za muziki kutokana na kushindwa kutumbuiza kwenye sherehe za mapinduzi zilizofanyika Aprili 26 katika Uwanja wa Maisala mjini Magharibi.

Zanzibar. Mwanamuziki Aslay amewaomba msamaha wakazi wa Zanzibar kupitia kwa Mkuu wa mkoa mjini Magharibi, Ayoub Mohamed baada ya kufungiwa kufanya shughuli za muziki ndani ya mkoa huo.

Mkuu wa mkoa huyo, ametoa katazo kwa Aslay kufanya shughuli za muziki kutokana na kushindwa kutumbuiza kwenye sherehe za mapinduzi zilizofanyika Aprili 26 katika Uwanja wa Maisala mjini Magharibi.

Akitangaza kuondoa katazo hili Mkuu wa mkoa huyo, amesema ameamua kumsamehe Aslay kutokana na  kuonyesha uungwana wa kuomba msamaha Wazanzibar Kwa ujumla  baada ya kushindwa kufanya shoo kwenye sherehe hizo. 

"Nimeamua kumsamehe Aslay kutokana na kufanya kitendo cha kiuungwana cha kuja kuomba msamaha kwa kosa alilofanya la kushindwa kuja kufanya shoo siku ya Mapinduzi ya Zanzibar

'Ni kweli niliweka katazo, nikamwambia Mkuu wa Jeshi, Aslay asifanye shoo ya aina yeyote hapa Mkoani kwani alionyesha kitendo cha dharau na kuwasababishia usumbufu wakati wa mkoani hapa," alisema  Ayoub

Naye Aslay amesema ameamua kuomba msamaha Wanzanzibar kutokana na kuwakosea kwa kushindwa kufika katika sherehe hizo, kwani alikuwa anaumwa.