Aslay aeleza sababu ya kuachia ngoma sita mfululizo

Muktasari:

  • “Kwa sasa naachia kazi nyingi kutokana na kwamba kipindi tukiwa Yamoto tulikuwa tunafanya sana kazi za kundi lakini kwa sasa kila mmoja anaweza kufanya kazi kivyake. Imenibidi niachie ngoma nyingi ili hata nikienda kufanya shoo niwe na nyimbo nyingi za kwangu,” alisema Asley

MSANII anayekimbiza kwa ngoma nyingi kwa sasa. Asley amefunguka kuhusu kuachia ngoma nyingi kwa kipindi kifupi kuwa ni kutokana na kutobanwa na shughuli za Yamoto Band ambapo nguvu kubwa awali ilikuwa huko.

“Kwa sasa naachia kazi nyingi kutokana na kwamba kipindi tukiwa Yamoto tulikuwa tunafanya sana kazi za kundi lakini kwa sasa kila mmoja anaweza kufanya kazi kivyake. Imenibidi niachie ngoma nyingi ili hata nikienda kufanya shoo niwe na nyimbo nyingi za kwangu,” alisema Asley

“Hivyo nitaendelea kuachia ngoma kali zaidi mpaka nitapoona hapa inafaa kusimama kwa muda basi nitasimama kwa muda ila watu waendelee kutegemea kazi kali zaidi,” aliongeza.

Mpaka sasa Aslay ameweza kuachia kazi zaidi ya sita ambazo zinaendelea kufanya vizuri katika vituo mbalimbali vya habari na kuendelea kukimbiza kwa watazamaji katika mtandao wa Youtube.