Olivier Giroud aokoa jahazi la Arsenal

Muktasari:

  • Arsenal imeweka kibindoni pointi 29 huku ikijiweka nafasi ya tano kabla ya mechi za leo kuhitimishwa.

 Mshambuliaji wa Arsenal, Olivier Giroud ameiokoa Arsenal ambayo jahazi lake lilikuwa linaelekea kuzama kwenye mechi ya Ligi Kuu England baada ya kuisawazishia bao la kichwa dakika za majeruhi dhidi ya Southampton.

Mchezo huo mkali  ambao Arsenal ilikuwa ugenini, vijana wa Wenger walipata bao la kusawazisha mbele ya Southampton walionekana kukomalia bao hilo lisirudi.

Hata hivyo, Giroud mtokea benchi hakufanya makosa baada ya kuchezeana vyema na Alexis Sanchez katika dakika ya 88 ya mchezo huo kipindi cha pili.

Licha ya Arsenal kumiliki mpira kwa kipindi kirefu lakini bahati haikuwa upande wao kuondoka na pointi tatu.