Arsenal kuuzwa leo kwa Mmarekani

Muktasari:

  • Bilionaire huyo wa Kimarekani anamiliki asilimia 67% ya hisa za Arsenal kupitia kampuni yake ya KSE, ambao wamesema Alisher Usmanov amekubali kuuza asilimia 30% ya hisa zake.

London, England. Mmiliki mkubwa wa hisa za Arsenal, Stan Kroenke ameweka dau la pauni 600milioni kwa lengo la kuinunua hisa zote na kufanya thamani ya Gunners kufikia thamani ya pauni1.8bilioni.

Bilionaire huyo wa Kimarekani anamiliki asilimia 67% ya hisa za Arsenal kupitia kampuni yake ya KSE, ambao wamesema Alisher Usmanov amekubali kuuza asilimia 30% ya hisa zake.

Taarifa ya KSE ilisema uamuzi wa kuichukua klabu hiyo kama mali binafsi itasaidia Arsenal katika kukamilisha mipango na malengo.

Uamuzi wa kununua hisa hizo utangazwa leo Jumanne katika soko la hisa la London.

Pamoja na kuwa mmiliki wa hisa hizo, Usmanov si mmoja wa wajumbe wa bodi inayofanya uamuzi ndani ya Arsenal.

Katika taarifa yake aliyotoa katika soko la hisa, Kroenke alisema KSE "imepiga hatua moja zaid kwa kuweka dau kubwa kwa lengo la kummiliki klabu hii kwa asilimia 100%" na kuongeza "tunampongeza Usmanov kwa kuamuzi wake" kwa ajili ya Arsenal.

Taarifa hiyo iliongeza kuwa: "KSE's lengo lake ni kuona klabu hiyo inafanya vizuri ikiwa ni kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England na Ligi ya Mabingwa, pamoja na kuchukua mataji yote muhimu katika soka la wanawake na timu za vijana pia."