Siku za Koeman zahesabika Everton

Muktasari:

  • Ushindi wa Arsenal imeipanda siku ya kuzaliwa kwa kocha Wenger

London, England.Kocha Everton, Ronald Koeman amekalia kuti kavu baada ya kushudia wachezaji wake 10 wakichezea

kichapo cha mabao 5-2 kutoka kwa Arsenal kwenye Uwanja wa Goodison Park.

Wachezaji wa Arsenal, Monreal, Ozil, Lacazette, Ramsey na Sanchez kila moja alifunga bao katika mchezo huo ambao kocha Arsene Wenger anasherekea kutimiza miaka 68 ya kuzaliwa kwake.

Kipigo hicho kinaifanya Everton kuporomoka hadi nafasi ya tatu kutoka mkiani wa Ligi Kuu England.

Wenyeji walianza mchezo huo kwa kishindo na kupata bao la mapema lililofungwa na Wayne Rooney katika dakika 12, kwa bao la shuti ambao linalofanana alilofunga miaka 15 iliyopita wakati akiwa na miaka 16 dhidi ya vijana wa Wenger.

Baada ya bao hilo Arsenal waliamka na kufanikiwa kusawazisha goli hilo kupitia Nacho Monreal dakika tano kabla ya mapumziko.

Arsenal iliendelea kulisakama bao la pinzani wao na kufanikiwa kupata bao la pili dakika 53, lililofungwa na Mesut Ozil.

Everton ilipata pigo dakika 63 baada ya mchezaji wao Idrissa Gueye kupewa kadi ya pili ya njano nakutolewa kwa kadi nyekundu.

Arsenal ilitumia mwanya huo kabla ya Alexandre Lacazette kupachika bao la tatu dakika 74, katika dakika za mwishoni Aaron Ramsey alifunga bao la nne kabla ya Alexis Sanchez kuhitimisha kalamu hiyo kwa kufunga bao la tano.

Wakati mashabiki wa Everton wakitoka uwanjani,  Oumar Niasse alifunga bao la pili kwa wenyeji na kufanya mchezo huo kumalizika kwa matokeo ya mabao 2-5.

Kipigo hicho kinamwacha kocha kocha Koeman akiwa njia panda kuhusu hatma yake.