Amissi Tambwe kufanya bonge la sherehe nyumbani

Muktasari:

Hata hivyo, katika kipindi cha mwezi huo, wamepanga kufanya sherehe ya maana itakayotingisha Jiji la Dar es Salaam na Afrika Mashariki kwa jumla. Katika sherehe hizo, unaambiwa kutafanyika fujo zote, kutapikwa chakula cha maana, vinywaji na kila kitu.

Watu na shughuli bwana! Mshambuliaji wa Yanga, Mrundi Amissi Tambwe na familia yake wamepanga kufanya sherehe ya maana mwezi wa Novemba.

Unajua sherehe hiyo ni ya nini? Iko hivi, sherehe hiyo ni harusi si unajua Tambwe na mkewe anayeitwa Ray walioana lakini ndoa hiyo ilikuwa ya ‘fasta fasta’ tu.

Hata hivyo, katika kipindi cha mwezi huo, wamepanga kufanya sherehe ya maana itakayotingisha Jiji la Dar es Salaam na Afrika Mashariki kwa jumla. Katika sherehe hizo, unaambiwa kutafanyika fujo zote, kutapikwa chakula cha maana, vinywaji na kila kitu.

Aliyedokeza ‘ishu’ zima ni mke wa Tambwe anayeitwa Ray:

“Tumejipanga kuona mambo yanakuwa mazuri, tumeanzaa sherehe mwezi wa 11.”