Ally Shomary aikomalia Kagame

Muktasari:

  • Shomary hakupata nafasi ya kuaminika ndani ya kikosi cha kwanza cha Simba mbele ya Shomary Kapombe na Mghana Nicholas Gyan ambao wanacheza nafasi moja kutokana na kuonyesha kiwango cha juu

Dar es Salaam. Beki wa kulia wa Simba, Ally Shomary amesema  katika michuano ya Kombe la Kagame inayotarajia kuanza Juni 29   itampa nafasi ya kuonyesha kiwango chake baada ya kushindwa kufanya vizuri kwenye ligi kuu.

Shomary hakupata nafasi mbele ya Shomary Kapombe na Mghana Nicholas Gyan ambao wanacheza nafasi moja kutokana na kuonyesha kiwango cha juu ndiyo maana akili yake ameigeuzia kwenye Kagame.

Simba tayari imeanza mazoezi ya kujiandaa na michuano hiyo chini ya kocha Mrundi Masoud Djuma, huku hatma ya mkuu wake, Piere Lechantre ikiwa haijulikani kama atabaki au ataondoka.

"Kwangu mimi naifurahia kwa sababu itanipa nafasi ya kuonekana, sikuwa na msimu mzuri wa ligi na nitakapofanya vizuri ninachokiamini ni kwamba kocha ataniamini upya,"alisema Shomary.

"Hii itanifanya msimu ujao wa ligi niwe na nafasi nzuri ya kucheza kwa sasa najituma na kujiandaa ili ninachokitarajia kifanikiwe,"alisisitiza Shomary.