Alliance FC wang’ara Ligi Daraja la Kwanza

Muktasari:

  • Alliance ilianza vyema michuano hiyo kwa kupata ushindi wa bao 1-0
  • dhidi ya Rhino ikiwa ugenini katika ligi ambayo ilianza kutimua vumbi jana Jumamosi.

Mwanza. Timu ya Alliance FC imesema kuwa ushindi walioupata kwenye mechi yake
ya kwanza ugenini dhidi ya Rhino Rangers kwenye Ligi Daraja la Kwanza
ni mwendelezo wao kuhakikisha hawapotezi mchezo wowote.
Alliance ilianza vyema michuano hiyo kwa kupata ushindi wa bao 1-0
dhidi ya Rhino ikiwa ugenini katika ligi ambayo ilianza kutimua vumbi jana Jumamosi.
Kocha Mkuu wa kikosi hicho, Mbwana Makata alisema kuwa ushindi huo ni
mwanzo mzuri na kwamba itakuwa mwendelezo wao kupata matokeo mazuri
ili kufikia malengo yao ya kupanda Ligi Kuu.
Alisema kuwa anaamini ligi Daraja la Kwanza kuwa na ushindani mkali, lakini maandalizi waliyoyafanya kwa vijana wake anaamini
watafanya vizuri.