AliKiba acheza mechi za Coastal Union jukwaani

Muktasari:

Coastal Union ni mabingwa wa Ligi Kuu bara mara mmoja walitwaa taji hilo 1988

Dar es Salaam. Mshambuliaji Coastal Union, mwanamuziki AliKiba ameendelea kutazama mechi za timu hiyo akiwa jukwaani tena leo dhidi ya African Lyon kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Jina la mwanamuziki huyo alikuwepo katika orodha ya wachezaji 18, walionza katika mchezo huo.

Hii ni mechi ya nne mfululizo kwa AliKiba kuitazama jukwaani licha ya usajili wake wa mbwembwe michezo mingine aliyokosa ni dhidi ya Biashara United, Lipuli na KMC.

Nyota 11 wa Coastal wanaoanza ni Hussein Sharrif, Ada Mohammed, Adeyum Ahmed, Ibrahim Mohammed, Bakar Mwamnyeto, Hassan Hamis, Muhsin Makame, Moses Kitandu, Hamis Kanduru, Haji Ugando na Issah Abushehe.

Refa wa kati ni Athuman Senkala akisaidiwa na Gasper Keto na Abdallah Uhako wanaotoka Arusha na mwamuzi wa akiba ni Mbaraka Rashid kutoka Dar es Salaam.

Kikosi cha African Lyon kilichoanza dhidi ya Lyon leo kinaundwa na wachezaji Dougras Kasebo, Halfan Mbaruku, Omary Salum, Daud Salum, Augustino Samson, Baraka Jafari, Ismail Gambo, Victor Da Costa, Haruna Moshi na Gervas Bernard.