African Lyon yaleta kocha Mfaransa achimba mkwara

Dar es Salaam. Kocha mpya wa African Lyon, Mfaransa Soccoia Lionel amesema mipango yake ni kuifikisha timu hiyo katika kiwango bora cha soka nchini.

Kocha huyo raia wa Ufaransa ameingia mkataba wa miaka miwili kuinoa timu hiyo iliyopanda Ligi Kuu msimu huu.

Akizungumza wakati wa kutambulishwa kwa waandishi wa habari Agosti 9, kwenye mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika katika uwanja wa Uhuru, kocha Lionel alisema anataka Lyon ijitofautishe na timu nyingine.

"Mpira kila mtu anaweza kucheza, lakini ni wa ufundi kiasi gani? nataka niitofautishe Lyon na timu za Tanzania kisoka, nahitaji kuona inacheza soka la ufundi na kuwa na mafanikio," alisema Lionel.

Kocha huyo aliambata na nyota mpya wa timu hiyo aliyetokea klabu ya Grenivik ya Iceland naye amesajiliwa kwa mkataba wa miaka miwili.

Meneja wa Lyon, Salehe Mkere alisema ujio wa kocha huyo umeongeza morali katika kikosi chao ambacho kimesajili nyota wapya 15 wakiwamo saba wa kigeni.

Wachezaji wengine ni Idriss Thobias wa Nigeria, kipa wa timu ya Taifa ya Uganda, Douglas Kisemba, Ibrahim Kawila, Udi Mayanja, Tito Okelo na Mike Ndera