20 wanasa mchongo SportPesa

Muktasari:

Watu hao walifanikiwa kushinda Promosheni ya Jiongeze na M-Pesa, Shinda na SportPesa iliyodumu kwa majuma 10 kuanzia Februari 9 mwaka.

KAMPUNI ya michezo ya kubashiri ya SportPesa imeendelea kuleta neema nchini baada ya kukamilisha zoezi la kutoa jumla ya pikipiki za miguu mitatu ‘Bajaj’ 20 kwa Watanzania 20 tofauti.

Watu hao walifanikiwa kushinda Promosheni ya Jiongeze na M-Pesa, Shinda na SportPesa iliyodumu kwa majuma 10 kuanzia Februari 9 mwaka.

Promosheni hiyo ambayo SportPesa ilifanya kwa ushirikiano na Kampuni ya Mawasiliano ya Simu za Mkononi ya Vodacom, iliwaruhusu wateja waliokuwa wakibashiri matokeo kupitia mtandao wa Vodacom pekee ambapo ilikuwa ikifanyika mara mbili kwa wiki katika siku za Jumatatu na Alhamisi.

Bajaji hizo 20 zilikuwa ni mwendelezo wa zawadi ya Bajaj nyingine 100 ambazo SportPesa ilizitoa kwa wateja wake katika Promosheni yake ya ‘Shinda na SportPesa’ iliyofanyika kwa kipindi cha siku 100 kuanzia Oktoba 26, 2017 hadi Februari 3 mwaka huu.

Washindi hao wa Bajaj 20 ambazo zilitolewa kupitia Promosheni hiyo ya Jiongeze na M-Pesa, Shinda na Sportpesa wanatokea katika Mikoa ya Mwanza, Mara, Rukwa, Kagera, Dar es Salaam, Mbeya, Iringa, Ruvuma, Shinyanga, Njombe na Kilimanjaro ambao walijipatia Bajaj hizo kwa nyakati tofauti.

Washindi hao ni Daudi Sima (36) kutoka Makete Njombe ndiye aliyefungua dimba kwenye droo ya kwanza iliyofanyika Februari 12, baada ya hapo washindi wengine walifuata ambao ni Edwin Victor (23), Aggrey Lauwo (19), Godfrey Magesa (37), Enock Sagwa (32), Yohana William (28), Richard Steven (23), Erasto Floridi (22), Joseph Nzary (32) na Gerald Christopher (25).

Wengine ni Paschal Raphael (24), Mathayo Edward (27), Majaliwa Hassan (29), Yohana Msigala (22), Juma Twike (35), John Mawela (32). Karim Prosper (29), Adam Obura (34), Linda Mwandu (32) na Awadh Hussein (28) ambaye ndiye amefunga dimba.

Miongoni mwa washindi wa Bajaji hizo 20, Yohana William mwenye umri wa miaka 28 kutoka Mwanza, alisema ushindi wa Bajaj hiyo utamsaidia kupata fedha za kuendeshea biashara na maisha yake kwa jumla.

“Bajaji hii itanikwamua katika maisha yangu kwasababu ndio mtaji mkubwa ambao nitaanza kuumiliki maishani mwangu tangu nimefika umri huu na kupitia Bajaj hii pia naweza kuendelea na masomo yangu,” alisema Yohana ambaye anafanya biashara ya kuuza kuku katika soko la Igoma mkoani humo.

Inatia moyo

Ushuhuda huo wa Yohana, ni moja kati ya shuhuda nyingi ambazo zinaifanya Kampuni ya SportPesa kupitia kwa Mkurugenzi wake wa Utawala na Udhibiti, Ndugu Tarimba Abbas kuamini promosheni hii imewainua Watanzania kiuchumi kwa kiasi kikubwa.

“Hakika ni jambo la kutia moyo kwetu sisi kama kampuni kuona jinsi ambavyo washindi hawa wakieleza namna ambavyo Bajaj hizi zitawainua kiuchumi.

“Mfano mzuri ni yule mshindi wa Mwanza (Yohana William) ambaye alisema kuwa Bajaj yake aliyoshinda itamuwezesha kurudi shule kujiendeleza na masomo.

“Tunapokuwa tunafikiria kuleta kampeni kama hizi huwa tunazingatia suala la kuinua kipato cha Mtanzania na pale tunapoona tumetimiza lengo hilo, basi kwetu huwa ni mafanikio makubwa sana,” alihitimisha Ndugu Abbas.

Mwisho tungependa kuipongeza Kampuni ya SportPesa kwa kuwapa Watanzania kipaumbele kwani kuendesha promosheni mbili kubwa ambazo zimegawa Bajaj 120 kwa Watanzania si jambo dogo.

SportPesa wameonesha mfano wa kuigwa, hivyo litakuwa ni jambo jema kama makampuni mengine nchini yangeiga mfano huu ili kuwawezesha vijana wengi wa Kitanzania kujiajiri.