Kuziona Yanga, Coastal ya Alikiba buku tano

Muktasari:

  • Yanga inakwenda katika mchezo huo ikiwa na rekodi ya kushinda mechi zake mbili za mwanzo

Dar es Salaam. Mashabiki wa Yanga wataishudia timu yao kesho Jumatano ikicheza na Coastal Union kwa kiingilio cha Sh 5,000 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam saa moja jioni.

Bodi ya Ligi kupitia Mkurugenzi wake, Boniface Wambura wametangaza viingilio vya mchezo huo leo.

Viingilio vya mchezo huo ni Sh15, 000 kwa VIP A, Sh10, 000 VIB B na C huku kijani na Machungwa ni Sh5000.

Wambura alisema viingilio hivyo vinatoa nafasi ya kila shabiki kuingia uwanjani na kushuhudia mechi hiyo kwenye Uwanja wa Taifa.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa wa kuvutia kutokana na mashabiki wengi kutarajia kumuona AliKiba akichezea timu yake ya Coastal Union kwa mara ya kwanza.