Mkuu wa Wilaya kushuhudia 'Papasa Square' ya Ruvu Shooting

Mtwara. Mkuu wa Wilaya ya Newala, Aziza Mangosongo anatarajiwa kuwepo katika mchezo wa kirafiki kati ya Ruvu Shooting dhidi ya Tandaimba City.
Mkuu huyo wa wilaya  amekubali wito wa Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire ambaye amemwomba muda mchache uliopita  awepo katika mchezo huo.
Ruvu Shooting imepanga kutumia mchezo huo wa kirafiki kama sehemu ya utambulisho wa mfumo wao mpya wa 'Papasa Square'.
"Asante sana Mheshimiwa na tutafurahi kukuona, tumepanga kutoa burudani kwa mashabiki wetu wapya," alisema Masau.
Zaidi ya mashabiki 100 kutoka kwenye halmshauri ya Newala mjini, vijijini na nje ya maeneo hayo wamenunua ticketi kwa ajili ya kuishuhudia Ruvu Shooting na  Afisa wake habari.
Mchezo huo wa kirafiki utachezwa kwenye uwanja wa Makonga na utashuhudiwa kwa kiingilio cha Tsh 2000.