Fernando Alonso kustaafu Formula 1

Dereva wa mbio za magari ya Formula 1, kutoka Kampuni ya magari ya McLaren, Fernando Alonso raia wa Hispania, ameamua kustaafu.

Alonso ambaye ametwaa ubingwa wa Dunia mara mbili amesema atastaafu mwishoni mwa msimu huu wa mashindano.

Dereva huyo mwenye miaka 37, alisema jana kuwa amepanga kustaafu baada ya kumalizika kwa mbio za Minardi katika mashindano ya Australian Grand Prix of 2001, akiwa ameshiriki kwa misimu 17 mfululizo na alitwaa ubingwa mwaka 2005 na 2006, akitumia gari aina ya Renault.

"Baada ya kashikashi za miaka 17, nimeamua kupumzika mbio za magari kilikua kipindi kigumu kwangu na kulikua na matukio ya kuhuzunisha na kufurahisha sasa ni muda wa kupumzika,” alisema.

Alisema kuwa uamuzi wa kustaafu aliufikia miezi kadhaa iliyopita kilichobaki ilikuwa ni kuutangaza hadharani tu.

Alonso alisema bado hajaamua ni kazi gani atakayoifanya katika maisha yake mapya ila akasisitiza kuwa hataficha kazi atakayoifanya.