Ruvu Shooting yapata mapokezi makubwa Newala

Muktasari:

Ruvu Shooting wanatarajia kufanya uzinduzi wa tawi lao kesho pamoja na kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Tandaimba City.

Mtwara. Msafara wa klabu ya Ruvu Shooting umewasili muda huu, Makonga wilayani Newala tayari kuanza ziara yao ya siku tatu.

Ruvu Shooting wanatarajia kufanya uzinduzi wa tawi lao kesho pamoja na kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Tandaimba City.

Wakazi wa eneo hilo, wamejitokeza kwa wingi kukishuhudia kikosi hicho ambacho msimu uliopita wa Ligi Kuu Tanzania Bara kilimaliza kwenye nafasi ya nane.

Nyota wa Ruvu Shooting waliopo kwenye ziara hiyo makipa ni Bidii Hussein, Jacton Robert, mabeki ni Abdul Mpambika, George Amani, Ally Mohammed, Hamis Kasanga, Renatus Kisase, Shaban Mtambo.

Viungo ni Zuberi Dabi, Baraka Mtuwi, Shabani Msala, Hamis Ismail, Chande Magoja, Adam Ibrahim na William Patrick. Washambuliaji ni Fully Zully, Abdallah Kulala na Mohammed Mdoe.

Nyota hao wameongozana na kocha wao mkuu, Abdulmutik Haji, msaidizi  Selemani Mtungwe,kocha wa viungo  Exsevia Owen, kocha wa makipa ni Godhald Misweku.

Daktari Simon Sugule, Meneja ni Augustine Palangwa, Afisa habari  Masau Bwire na mkuu wa msafara ni Captain Stanley Chahe.