Cannavaro aifutia nuksi Yanga ikishinda bao 1-0

Timu ya Yanga imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mawenzi Market FC kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Jamhuri Morogoro leo Jumapili.

Bao la Yanga liliwekwa wavuni dakika ya 53 na Heritier  Makambo jambo ambalo liliwainua mashabiki wa Yanga waliokuwa wamefurika uwanjani hapo.

Tukio la kuvutia uwanjani hapo ilikuwa na kuangwa kwa aliyekuwa nahodha wa timu hiyo Nadir Haroub 'Cannavaro' ambaye alicheza dakika 10 za kipindi cha kwanza kisha kutoka nje.

Tukio hillo liliwaacha na huzuni wachezaji ambapo walimkumbatia kabla ya kutoka nje ya uwanja huku akimkabidhi nafasi ya unahodha beki kisiki Kelvin Yondani.

Yanga imeweka kambi mkoani Morogoro kwa ajili ya maandalizi ya msimu huu.