Kiungo Bandari aitupia madongo Gor Mahia

KIUNGO wa Bandari ya Kenya, Abdallah  Hamisi amesema kipigo walichowashushia  Gor Mahia  cha mabao 2-1, kimeonyesha ubora wa kikosi chao ambacho jana kilikuwa na mchezo wa Ligi Kuu nchini humo  dhidi ya Tusker.

Hamisi alikuwa mwiba mkali kwenye eneo la kiungo kwa kuharibu mipango ya Gor Mahia ambao wamezoeleka kutengeneza mashambulizi yao kupitipia eneo hilo na pembeni kwa mawinga.

“Tulijiandaa kushinda ili tusogee kwenye nafasi za juu zaidi na kilichotusaidia ni  maandalizi tuliyoyafanya, upande mwingine ushindi ule umetufanya kupunguza idadi ya pointi kati yetu na wao,” alisema kiungo huyo mkabaji.

Bandari imeweka rekodi kwa kuwa timu ya kwanza kuifunga Gor Mahia ambao mchezo huo ulikuwa wa 24 kwenye muendelezo wa mechi zao za Ligi Kuu Kenya.