Perez amchungulia staa Hazard kwenye rada

MADRID, HISPANIA
RAIS wa Real Madrid, Florentino Perez amemwambia bosi mwenzake wa Manchester United, Ed Woodward kwamba amefuta mpango wote wa kumsajili winga wa Chelsea, Eden Hazard.
Ripoti zinadai kwamba Perez alikutana na Woodward mjini Miami, Marekani walipokuwa na mazungumzo ya kuhusu uwezekano wa Man United kumsajili beki wa kati Raphael Varane ndipo hapo bosi huyo wa wababe wa Hispania alipocheza kwamba hawafikirii tena kumchukua Hazard.
Real Madrid kwa muda wamekuwa wakimfukuzia staa huyo wa Chelsea na siku za karibuni jambo hilo limeshika kasi zaidi baada ya Los Blancos kumpoteza staa wao Cristiano Ronaldo, aliyetimkia Juventus. Hata hivyo, Chelsea iliweka mambo wazi kwamba hawana mpango wa kumuuza Hazard licha ya mchezaji mwenyewe kuonekanna kuutamani uhamisho huo.
Lakini, kwa sasa mpango huo sasa unaonekana haupo tena kwa sababu Perez alimwambia Woodward, ambaye ni makamu mwenyekiti wa Man United kwamba hawamsajili Hazard tena.